CPA MOREMI MARWA ATEMBELEA BANDA LA TTCL ARUSHA
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, ametembelea Banda la Maonesho la Shirika hilo lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) na kupokelewa na Mkurugenzi wa Biashara Bw. Vedastus Mwita.
Bw. Mwita alimweleza Mkurugenzi Mkuu jinsi Shirika hilo linavyotimiza wajibu wake wa kuhakikisha huduma za Mawasiliano zinawafikia Watanzania wote na hivyo kuleta maendeleo endelevu.
Aidha alimweleza Shirika hilo linavyojipambanua katika utoaji wa huduma ya Intaneti ya kasi ili kuendana na Mpango Mkakati wa Serikali wa utoaji wa huduma kidigitali ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi.
CPA Marwa alitembelea banda hilo wakati akishiriki Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kilichoanza Agosti 27,2024 ambapo kinatarajiwa kumalizika Agosti 30 Mwaka huu jijini Arusha.
Kikao hicho cha siku nne kilichoandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina kimefunguliwa rasmi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.