info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

SABA SABA 2024 FURSA KWA TTCL KUONESHA UMAHILI WAKE SEKTA YA MAWASILIANO

Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL linashiriki katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Hii ni fursa kubwa kwa TTCL kuonesha bidhaa zake za mawasiliano, kutoa elimu kwa umma, na kuimarisha uwepo wao katika sekta ya biashara na mawasiliano hapa nchini. 

Maonesho haya ni muhimu sana kwa kuunganisha wadau mbalimbali na kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo TTCL kama mdau muhimu wa maendeleo ya uchumi na kijamii kidigitali uwepo wake katika maonesho haya unawapa fursa Wafanyabiasha, Wajasiriamali pamoja na Wananchi kwa ujumla kujua zaidi kazi na huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Aidha Maonesho haya ya Kimataifa ya Biashara Saba Saba ni fursa kubwa kwa TTCL kushiriki na kuonesha inachangia kwa kiasi gani katika kukuza na kuendeleza sekta mbalimbali katika mabadiliko ya kiteknolojia.

TTCL inatumia uwepo wa maonesho haya kuonesha bidhaa zake za mawasiliano kama vile simu, intaneti, na huduma za data kwa wateja na wadau wengine.

Vile vile ni fursa ya kutoa elimu kuhusu Huduma kwa wateja na kwa umma kuhusu huduma za mawasiliano, mabadiliko ya kiteknolojia, na jinsi ya wananchi wanavyonufaika nazo.